Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 4, 2018

KAMATI YA UONGOZI YA CHAMA CHA MASPIKA WA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA KANDA YA AFRIKA(CPA-AFRIKA) MJINI ZANZIBAR!

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza na Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (Mb), (Wa kwanza kushoto) na Ujumbe wake ambao ni Kamati ya Uongozi ya Chama cha Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika(CPA-Afrika) waliokwenda kumtembelea leo Ikulu Zanzibar. Wa pili kushoto ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Zuberi Ali Maulid, Naibu Spika wa Bunge la Rwanda Mheshimiwa Edda Mukabagwiza na Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (Mb) (kushoto) na Naibu Spika wa Bunge la Rwanda Mheshimiwa Edda Mukabagwiza (kulia) mara baada ya kuzungumza nao Ikulu Zanzibar.

Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (Mb) akiongoza kikao cha Kamati ya Uongozi ya Chama cha Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika(CPA-Afrika) kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Tunguu, Zanzibar. Wa kwanza kutoka kulia ni Spika wa Bunge la Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Zuberi Maulid, Spika wa Bunge la Sierra Leone Dkt. Abbas Bundu na Naibu Spika wa Bunge la Rwanda Mheshimiwa Edda Mukabagwiza.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (Mb) (wa tatu kutoka kushoto) katika picha ya pamoja na Wajumbe Kamati ya Uongozi ya Chama cha Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika(CPA-Afrika. Kutoka (kushoto) kwa waliokaa ni Katibu wa Bunge Ndg. Stephen Kagaigai, Naibu Spika wa Bunge la Rwanda Mheshimiwa Edda Mukabagwiza, Spika wa Bunge Bunge la Sierra Leone Dkt. Abbas Bundu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Zuberi Maulid na Katibu Msaidizi wa CPA-Afrika Ndg. Demetrius Mgalami. Waliosimama ni Sekretarieti ya Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika(CPA-Afrika).
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Zuberi Maulid (katikati) wakati alipotembelea Baraza hilo kabala ya kuanza kwa kikao cha Kamati ya Uongozi ya Chama cha Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika(CPA-Afrika) kinachoendelea Mjini Zanzibar. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge la Rwanda Mheshimiwa Edda Mukabagwiza.
PICHA NA BUNGE

No comments :

Post a Comment