Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Godbless Lema ameitwa kuripoti katika Kituo Kuu cha Polisi jijini Arusha bila kukosa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram na Twitter, Lema ameandika " Nimepigiwa simu na Polisi kwamba natakiwa kuripoti kituo kikuu cha Polisi Arusha leo (jana) bila kukosa, sijaelezwa sababu lakini wito unaonekana kuwa wa lazima sana, lakini nafikiri kupigania haki ndio linaweza kuwa kosa langu kubwa. MSIOGOPE."
Muda mchache baada ya Lema kuandika ujumbe huo Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe aliandika maneno haya chini ya ujumbe wa Lema.
" Wewe kama Waziri Kivuli Mambo ya Ndani umetimiza wajibu wako kupinga utekaji. Watanzania wanajua na Dunia inajua. Wajibu wa Polisi ni kulinda raia na sio kutisha raia. Wajibu wa Mbunge ni kuisimamia serikali likiwemo jeshi la Polisi. Tutashinda". ameandika Zitto.

No comments :
Post a Comment