Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 25, 2018

Madaktari wateswa na Ugonjwa usiojulikana!

Madaktari katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, wanaumiza vichwa kutafuta sababu ya vifo vya wananchi katika kijiji cha Namasalau wilayani humo.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Prosper Ponera, alisema juzi kuwa hali hiyo imetokana na timu ya kwanza ya wataalamu ambayo ilitumwa kwenda kufanya uchunguzi katika vyanzo vya maji na kuchukua sampuli za damu kutoka kwa baadhi ya wananchi, kutobaini chanzo cha ugonjwa huo.Dk. Ponera alisema wataalamu hao walifanya utafiti katika vyanzo vya maji wakiwa na uhakika kuwa huenda maeneo hayo yangekuwa miongoni mwa vyanzo vya ugonjwa wa kuhara na kutapika damu, uliosababisha vifo hivyo.

Alisema uchunguzi huo ulifanyika kutokana na kuwapo kwa vifo vilivyodaiwa kuwa chanzo chake ni mlipuko wa homa ya matumbo ambayo ilikuwa ikisababisha baadhi ya wananchi kuhara na kutapika damu na baadaye kupoteza maisha katika kipindi kifupi.

Kwa mujibu wa mganga mkuu huyo, uchunguzi wa wataalamu hao ulibaini kuwa wagonjwa wawili waliodaiwa kutibiwa katika hospitali ya wilaya na kupona walibainika kuugua kifua kikuu (TB) ambao ulishafikia katika hatua ya kukomaa, hivyo kuwafanya wagonjwa kutoa makohozi yalichanganyika na damu.

Kutokana na hali hiyo, alisema tayari wagonjwa hao wamekwishaanzishiwa dawa ya  kifua kikuu na kwamba uchunguzi zaidi unaendelea kwa kutoa elimu kwa wananchi wa kijiji hicho ikiwa ni pamoja na kuwashauri kuzingatia kanuni za afya na usafi.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na mwandishi wa habari hii kijiji hapo, walidai kuwa wananchi hao walifariki dunia kuanzia Septemba 30, mwaka huu baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Juma Homera, alisema atawaagiza wataalamu wa afya kwenda tena kijijini hapo, ili kufanya uchunguzi zaidi kufuatilia hali ya usafi katika maeneo ya wananchi ikiwamo ukaguzi wa vyoo.

No comments :

Post a Comment