Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wadau wa utalii katika mchapalo ulioandaliwa na Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale katika hoteli ya Park Hyatt Zanzibar jana jioni tarehe 17, Oktoba 2018. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wadau mbalimbali wa utalii katika mchapalo ulioandaliwa na Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale katika hoteli ya Park Hyatt Zanzibar jana jioni tarehe 17, Oktoba 2018. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Sekta ya Utalii imeendelea kukua kwa kasi sana Duniani kutokana na maendeleo ya teknolijia na upatikanaji taarifa.
Makamu wa Rais aliyasema hayo jana jioni wakati alipokutana na Wadau wa sekta ya utalii katika Mchapalo ulioandaliwa na Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.
Sekta ya Utalii imeendelea kukua ambapo mwaka 2017 zaidi ya Watalii 433,474 waliitembelea Zanzibar ambao ni asilimia 32 zaidi ukilinganisha na mwaka 2014.
Idadi ya Watalii walioandikishwa kwa Tanzania nzima ni milioni mbili kwa mwaka 2017 ikilinganishwa na milioni 1.28 mwaka 2016.
Makamu wa Rais amesema kuwa ujenzi wa mahoteli, kuongezeka kwa ndege, na juhudi za kukuza masoko kunakufanya Zanzibar kuwa eneo zuri zaidi linalovutia watalii.
“Tunahitaji wawekezaji binafsi ili kupanua na kuendelea kuboresha Utalii, kwa kufanya hivyo, tunahitaji kuwezesha miradi kubwa ya uwekezaji. Aidha, kufikia ukuaji wa juu wa utalii ni jitihada za pamoja, ambapo ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi ni muhimu.” alisema Makamu wa Rais.
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Mahmoud Thabit Kombo alimshukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuhudhuria Tamasha la Kimataifa la Utalii Zanzibar 2018 (Zanzibar Tourism Show 2018) ambapo aliuambia umma wa shughuli hiyo kuwa Mhe. Samia ni mmoja wa msingi muhimu wa ukuaji wa Utalii Zanzibar.
|
No comments :
Post a Comment