Wanasayansi nchini Uingereza na Gambia wanasema wana ushahidi wa awali unaoonesha kuwa mbwa wanaweza kunusa malaria.Wanasayansi hao wamewafunza mbwa kutambua harufu ya malaria kwa kutumia nguo za watu wenye maambukizi.
Kuna matumaini makubwa kuwa wanyama hao watatumika katika mapambano dhidi ya malaria na hatimaye kuutokomeza kabisa ugonjwa huo.Japokuwa utafiti huo upo katika hatua za awali, wanasayansi wanaamini matokeo yake yanaweza kubadili namna ya kufanya vipimo vya malaria.
Kwa mujibu wa tafiti za hapo awali, mtu ambaye ana vimelea vya malaria mwilini anakua na harufu ya tofauti ambayo inawavutia mbu kuendelea kumshambulia. Na sasa, mbwa wapo kazini kuinusa harufu hiyo.
Japokuwa utafiti huo upo katika hatua za awali, wanasayansi wanaamini matokeo yake yanaweza kubadili namna ya kufanya vipimo vya malaria.
Kwa mujibu wa tafiti za hapo awali, mtu ambaye ana vimelea vya malaria mwilini anakua na harufu ya tofauti ambayo inawavutia mbu kuendelea kumshambulia. Na sasa, mbwa wapo kazini kuinusa harufu hiyo.
No comments :
Post a Comment