Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa chama cha wananchi CUF Taifa, Juma Duni Haji amesema wataendelea kuthamini jitihada zinzofanywa na wanawake wa chama hicho katika kuhakikisha chama kinaendelea kusonga mbele
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza katika mkutano mkuu wa mkoa wa jumuiya ya wanawake CUF huko bumbwini mkoa wa kaskazini unguja na kusisitiza kuendelea kua na umoja na mshikamanoili kuendelea kukiimarisha chama hicho.
Amesema juhudi za wanawake katika chama hicho haziwezi kupingwa kutokana na wao kua ndio waletaji wakubwa wa mabadiliko na maendeleo katika nchi hivyo juhudi zao zinapawa kuthaminiwa
Duni ambaye pia ni mgombea mwenza wa Urais mwaka 2015 kupitia Chadema, amewataka wanachama hao kuwa wasthamilivu na wasikubali kufanya jambo lolote kinyume na utaratibu wa chama chao huku wakisubiria kupata neema katika kipindi kifupi.
Kwa upande wake mlezi wa jumuiya ya wanawake CUF wilaya ya kaskazini Ashura Sharif Ally amewataka wanawake wa chama hicho kuachana na ubaguzi li kuweza kujenga umoja upendo na mshikamano katika chama chao.
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

No comments :
Post a Comment