MAHAKAMA nchini Korea ya Kusini imemhukumu kifungo cha miaka 15 jela na kumwamru kulipa faini ya dola milioni 11.5 aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Lee Myung-bak (76) baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya rushwa.
Lee anakuwa Rais wa nne wa nchi hiyo kuhukumiwa kutumikia kifungo jela baada ya wengine watatu kufungwa kwa makosa ya rushwa akiwemo mtangulizi wake, Park Geun-hye ambaye alifungwa miaka 33 jela.
Mwanasiasa huyo ambaye aliingia madarakani Februari 25, 2008 hadi Februari 25, 2013, alithibitika kutenda kosa hilo wakati wa uongozi wake baada ya kupokea kiasi cha dola milioni 10 kutoka kwa kampuni ya Samsung na wakati wote wa kesi hiyo, Lee alikuwa akikana mashtaka hayo na kusema kuwa yamechagizwa kisiasa.
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment