Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 24, 2018

Nyalandu ahutubia mkutano wa Chadema, afichua siri za CCM!


Kada mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Lazaro Nyalandu amefichua mbele ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe sababu za yeye kukaa kimya kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu ajiunge nao akitokea Chama cha Mapinduzi CCM huku pia akimtaka Mbowe kuwa shujaa na asiogope.

Ameyasema hayo katika mkutano wa ndani wa chama hicho mkoani Shinyanga ikiwa ni muendelezo wa kunadi sera zao mbadala.

Nyalandu amesema aliamua kukaa kimya kwa kipindi chote hicho ili kusubiri wakati sahihi ambao ilibidi ufike wa yeye kuanza kukitumikia chama hicho kikuu cha upinzani.

" Mimi ni toleo jipya, mimi ni yuleyule ambaye katika tarehe ile ile nilisimama katika siku ambayo hawakutarajia na pengine hamkutarajia baada ya kutafakari sana nikaamua kuondoka juhudi nilikua naziona lakini zilikua hazitoshi, nikaamua kuondoka ili kuunga mkono mabadiliko.

" Na baada ya mwaka mmoja hata Mwenyekiti (Mbowe) aliulizwa na watu wengine waliuliza, Nyalandu yupo wapi? maana alikuja halafu akapotea na nikawaambia kulikua na saa ambayo ilikua lazima ifike, na ile saa ni jana na ndio ilikua ni mra ya kwanza kuvaa gwanda, mara ya kwanza kukaa kingangari na kuwa tayari katika hili zoezi," amesema Nyalandu.

Nyalandu amefichua siri kuwa kipindi akiwa CCM walikua wakiiogopa Chadema huku akisema walikua hawalali wakihakikisha wanapanga mipango ya kuwashughulikia.

" Mimi si nilikua Mwenyekiti wa Vijana Mkoa, sijui Mbunge? Mzee Sumaye yupo hapa atasema tulikua tukisikia Chadema wanakuja tunaogopa tunapanga mipango ya kuwashughulikia, Easter Bulaya yupo hapa atawaambia kuna siku alikuja akatukuta tunapanga mipango ya kuwazuia Chadema lakini leo Chadema wamekua waoga, wanaogopa hata kuvaa sare zao.

" Wakati mwingine tunapita katika majaribu, moyo wako unaguswa wanachadema wengi wanapatwa mashaka, wabunge wana hofu na ubunge wao, kila mwanachadema simama kama shujaa, watazame wale waliosimama uwezeshwe kuwaona watu sawasawa uwaone watu kama walivyo, utashangaa sisi si CCM tulikua tunawaogopa nyie mnafikiri hatuwaogopi, kumbe unadili na waoga watupu, unadili na watu wanaojijua hawana kura kabisa, ushindi upo mikononi mwenu, " amesema Nyalandu.

No comments :

Post a Comment