Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 30, 2018

Rais Magufuli atumiwa ujumbe na Kafulila!


Katibu tawala wa Mkoa wa Songwe David Kafulila amesema anafurahia kufanya kazi na kiongozi wa nchi kwa kile alichokidai amekuwa mtu wa kufanya maamuzi.

Kafulila ametoa ujumbe huo ikiwa leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Kafulila amesema “ninamuombea kwa Mungu amzidishie maisha marefu na azidi kumjenga kwenye haya anayosimamia, kuna mambo mengi ambayo kipindi chake yeye yanatakelezeka sana, hasa kwenye usafiri wa anga na miundombinu mingine”.

“Kazi yangu ya utendaji hasa zama za Magufuli imekuwa nyepesi kwa mtendaji mwaminifu, na hasa ukiwa mtendaji ambaye hupendi rushwa, mi nafurahia sana nipo kwenye utendaji, ningekuwa kwenye ubunge ningependekeza lakini mimi kama mtendaji ninatakiwa kufanya maamuzi.”Ameongeza Kafulila

Julai 28 mwaka huu Rais Magufuli alitangaza kuwateua baadhi ya makada waliokuwa wamehama kutoka upinzani na kujiunga na CCM kwa nia ya kumuunga mkono, akiwemo Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi, Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Moses Machali na David Kafulila kama Katibu Tawala wa Songwe.

No comments :

Post a Comment