RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein ameipongeza Jumuiya ya Madola kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar na kuwapongeza Maspika wa Mabunge ya Jumuiya hiyo wa nchi za Afrika kwa kuja kufanya vikao vyao hapa Zanzibar.
Dk. Shein ameyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar wakati alipokutana na viongozi wa Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola wa nchi za Afrika wakiongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye Mwenyekiti wa Maspika hao hivi sasa Job Ndugai aliyefuatana na mwenyeji wake Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid.Katika maelezo yake Rais Dk. Shein alieleza kuwa Jumuiya ya Madola inathamini na kutambua juhudi kubwa inazozichukua Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo Zanzibar katika kuiendeleza na kuiimarisha Jumuiya hiyo yenye historia kubwa.
Aidha, Rais Dk. Shein alipongeza juhudi za Jumuiya ya Madola za kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuendeleza na kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo.
Aliongeza kuwa mnamo mwezi Agosti mwaka jana Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi Baroness Patricia Scotland alitembelea Zanzibar na kufanya nae mazungumzo ambapo Katibu huyo aliahidi kuwa Jumuiya hiyo itaendelea kuiunga mkono Zanzibar kwa kutambua juhudi inazozichukua katika kujiletea maendeleo.
Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi zake za pekee kwa Maspika wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola Barani Afrika kuja Zanzibar kwa ajili ya kufanya mkutano wao wa maandalizi ya Mkutano Mkuu.
Rais Dk. Shein alieleza kuwa kutokana na anavyomfahamu Spika huyo wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jinsi alivyomchapa kazi na mwenye ari, juhudi na maarifa katika utendaji wake wa kazi anaimani kubwa Jumuiya hiyo itazidi kupata maendeleo.
Dk. Shein alisema kuwa kufanyika kwa mkutano huo hapa Zanzibar ni fursa moja wapo ya kuendelea kuitangaza Zanzibar kiutalii ambapo Rais Dk. Shein aliwakaribisha viongozi hao wote wakiwemo Maspika wa Jumuiya hiyo kuja kutembea Zanzibar.

No comments :
Post a Comment