Ujerumani, Ufaransa na Uingereza kwa pamoja zimetoa wito zikitaka uchunguzi wa kina ufanyike kuhusiana na kutoweka kwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Jeremy Hunt , Jean-Yves Le Drian wa Ufaransa na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas.
Ufalme wa Saudi Arabia unasema tuhuma dhidi yake kuhusiana na suala la Khashoggi hazina msingi. Hata hivyo ufalme huo haujatoa ushahidi unaoonesha mwandishi huyo wa habari ambaye amekuwa akimkosoa mfalme wa Saudia Mohammed bin Salman kama aliondoka katika ubalozi wa mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul.
Ikulu ya Marekani imepuuza vitisho vya Saudi Arabia kwamba huenda ikalipiza kisasi kwa hatua yoyote ya Marekani kuiadhibu kichumi falme hiyo, kuhusiana na tuhuma za mauaji ya mwandishi Khashoggi, huku ikitoa wito wa uchunguzi ulio wazi kuhusiana na kutoweka kwake.
Maseneta wawili wa chama cha Republican, wamesema bunge la Marekani liko tayari kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kuzuwia uuzaji silaha kwa Saudi Arabia.
No comments :
Post a Comment