Seneta Bernie Sanders atolea wito Marekani kuacha kuiunga mkono Saudia kwa kukiuka haki za binadamu YemenSeneta Bernie Sanders asema kuwa Marekani inatakiwa kuacha kuinga mkono Saudia kutokana na kukiuka haki za bianadamu nchini Yemen.
Akizungumza kuhusu mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi , Bernie ametolea wito Marekani kuacha kuiunga mkono Saudia kwa kukiuka haki za binadamu katika vita vya Yemen.
Katika taarifa zilizochapishwa katika jarida la The New York Times, Bernie amenukuliwa akisema kuwa Saudia inatakiwa kufahamu kuwa haifumbiwi macho kwa ukiukwaji wake wa haki za binadamu nchini Yemen.
Kwa mujibu wa Sanders jambo la kwanza muhimu kuzuia ukiukwaji wa haki za binadamu Yemen ni Marekani kuacha kuiunga mkono Saudia.
No comments :
Post a Comment