Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametoa maelezo ya kwanza rasmi juu ya mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul. Amesema mauaji hayo yalipangwa.
Rais Erdogan alianza kwa kuwapa pole familia ya mwandishi Jamal Khashoggi na raia wa Saudi Arabia kwa jumla kisha aliendelea kueleza yale yote yaliyotokea kabla na siku mwandishi huyo alipofika kwenye ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul.
Amesema mpango wa mauaji hayo ulianza kuandaliwa mnamo tarehe 29 mwezi Septemba. Erdogan amesema kamera za ubalozini hapo ziliondolewa kabla ya mauaji hayo na siku moja kabla ya mauaji hayo wataalamu wa uchunguzi wa jinai waliwasili mjini Istanbul.
Khashoggi aliuawa tarehe 2 Oktoba. Erdogan pia amesema baada ya Khashoggi kuuawa mmoja wa watu hao alivaa nguo zake na kutoka ubalozini ili aonekane kuwa mwandishi huyo alitoka ubalozini hapo.
Rais Erdogan ameutaka utawala wa kifalme uwataje wote waliohusika na mauaji ya Jamal Khashoggi. Katika hotuba yake rais Erdogan amesema wauaji hao wa Saudi Arabia walirekodi kila kitu na ameuliza uko wapi mwili wa Jamal Khashoggi?. Wakati huo huo Erdogan ametaka washukiwa 18 waliokamatwa nchini Saudi Arabia waletwe Uturuki kujibu mashtaka ya kumuua Jamal Khashoggi.

No comments :
Post a Comment