Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, October 21, 2018

Sugu kumwaga Milioni Moja, Ni kwa atakayemletea Picha hii!

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu ametangaza dau la Tsh Milioni  1 kwa mtu yeyote atakayempatia picha yake akiwa amevalia sare za Gerezani kipindi alivyokuwa amefungwa.

Sugu ametoa tangazo hilo kwenye ukurasa wake wa Instagram, ambapo ameeleza kuwa lengo kubwa la picha hiyo ni kutumika kama Cover ya kitabu chake kipya cha ‘SIASA NA MAISHA’ .

“Kwa kweli bado mpaka sasa hivi sijampata, najua wanakataza kupiga picha jela  ndio maana nimetoa tangazo kama kuna mtu anayo, na sitamtaja, na ndio maana tunataka kwa njia ya email, ninachotaka ni picha kwa ajili ya kukamilisha kitabu chetu”, amesema Sugu.

Sugu ameendelea kwa kusema kwamba, ”muitikio umekuwa mkubwa lakini picha bado hatujaipata, inanitia moyo watu wanataka kushiriki katika kukamilisha hiki kitabu, hii hata kama ni askari jela alinipiga picha kwa mizuka yake, nao wanaruhusiwa kutuma ile picha kwenye email yangu ambayo ni deiwaka14@gmail.com na hatutamtaja”.

No comments :

Post a Comment