Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, October 26, 2018

UINGEREZA: ALIYEMUUA LEYLA KUHUKUMIWA LEO, WATANZANIA WAFURIKA KORTINI!

HUKUMU ya kesi ya inayomkabili Mtanzania Kema Salum (39) anayedaiwa kumuua mkewe ambaye pia alikuwa Mtanzania, Bi. Leyla Mtumwa (36), imetarajiwa kutolewa jana Alhamisi, Oktoba 25, 2018 katika Mahakama ya Old Bailey, mjini London nchini Uingereza.

Salum anashikiliwa jeshi la oolisi nchini Uingereza kwa tuhuma hizo ambazo anadaiwa kumuua Leyla kwa kumchoma visu kifuani na shingoni mnamo Machi 30, 2018 alfajiri, eneo walilokuwa wakiishi, Kirkstall Avenue, Haringey, baada ya kugombana na mkewe huyo.


Septemba 24, Salum ambaye anawakilishwa na wakili wake, Seona White, alikiri kumuua Leyla ambapo kesi hiyo ilipangwa kutolewa hukumu Oktoba 5 mwaka huu, lakini ilipowadia siku hiyo, hukumu ilisogezwa mbele na kupangwa kutolewa jana Oktoba 25.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Global TV Online aliyepo mahakamani hapo, mpaka sasa mama wa Leyla, Bi. Hidaya, ameshafika mahakaman na marafiki wa marehemu na Watanzania wengine wengi kusikiliza hukumu hiyo ambayo imevuta hisia ya watu wengi.

Baada ya uchunguzi wa polisi jijini London, mwili wa Leyla ulisafirishwa hadi nyumbani kwao Tanzania, mkoani Arusha ambako ulizikwa Aprili 24, 2018


GPL

No comments :

Post a Comment