Watu 19 kati ya 26 waliokuwa wakishikiliwa na polisi wakihusishwa na tukio la kutekwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ wameachiwa kwa dhamana jana usiku Oktoba 15, 2018.
Miongoni mwa walioachiwa ni Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara aliyekamatwa Oktoba 12, 2018 kutokana na kusambaza taarifa za tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii kwa madai ya kutumwa na familia jambo ambalo si kweli.
Kauli ya kuachiwa kwa watu hao imetolewa leo Jumanne Oktoba 16, 2018 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.
Mambosasa amesema kufuatia kuachiwa kwa watu hao, polisi inaendelea kuwashikilia wengine saba. Hadi jana mchana watu 26 waliokuwa wakishikiliwa na polisi.
No comments :
Post a Comment