Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, October 26, 2018

Waliosambaza video chafu kuchukuliwa hatua!

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza amesema wameanza kuwachukulia hatua wasanii wote waliovujisha video zenye maudhuhi ya picha za ngono mitandaoni, kwa mujibu wa sheria na miongozo iliyopo, bila kuangalia nani aliyefanya.

Akiongea na 'EATV SAA MOJA'  juu ya suala hilo, Naibu Wazir amesema Wema Sepetu tayari ameitwa na bodi ya filamu na kufanyiwa mahojiano kwa kusambaza picha zenye mahudhui ya kingono, na wasanii wengine ambao wamefanya makosa kama hayo pia watachukuliwa hatua.Mhe. Shonza ameendelea kwa kusema kwamba mpaka sasa Baraza la Sanaa Tanzania, (BASATA) halimtambui mtu anayejiita 'Amber Ruti' kama ni msanii, kutokana na kutosajiliwa na baraza hilo.

Licha ya hayo Mh. Shonza amesema kwamba wasanii hao pia wataitwa na TCRA, huku akiwataka wasanii kutumia mitandao kuelimisha jamii badala ya kubomoa maadili na tamaduni za kitanzania.

No comments :

Post a Comment