Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama eneo lililoandaliwa kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Kuzalisha Umeme katika Maporomoko ya Mto Rufiji- Stieglers Gorge wakati alipotembelea eneo hilo Oktoba 4, 2018. Kushoto kwake ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kutembelea eneo la ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Moporomoko ya Mto Rufiji – Stieglers Gorge, Oktoba 4, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Tanzania wa TAZARA, Fuad Abdallah wakati alipotembelea Stesheni ya TAZARA ya Fuga kukagua ujenzi wa tawi la reli hiyo litalounganisha steheni hiyo na eneo utakapojengwa Mradi wa Umeme wa Maporomoko ya mto Rufiji – Stieglers Gorge, Oktoba 4, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo wakati alipowasili kwenye eneo utakapojengwa Mradi wa Umeme katika Maporomoko ya Mto Rufiji - Stieglers Gorge, Oktoba 4, 2018. Kulia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka wa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) kuhusu ujenzi wa tawi la reli litakalounganisha Stesheni ya Fuga katika reli ya TAZARA na eneo utakapojengwa Mradi wa Umeme wa Maporomoko ya Mto Rufiji – Stieglers Gorge wakati alipotembelea eno hilo Oktoba 4, 2018. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Tanzania wa TAZARA, Fuad Abdallah.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa tawi la reli litakalounganisha Stesheni ya Fuga katika reli ya TAZARA na eneo utakapojengwa Mradi wa Umeme wa Moporomoko ya Mto Rufiji – Stieglers Gorge wakati alipotembelea Stesheni hiyo, Oktoba 4, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Tanzania wa TAZARA, Fuad Abdallah. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Eneo litakapojengwa tuta la kukinga maji katika Mradi wa Kuzalisha Umeme kwenye Maporomoko ya Mto Rufiji- Stieglers Gorge ambalo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alilitembelea, Oktoba 4, 2018.
No comments :
Post a Comment