Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 18, 2018

Zitto Kabwe aibua mengine kutekwa kwa MO Dewji, aungana na Lema!


Siku moja baada ya Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Godbless Lema kujitokeza hadharani kuzungumzia suala la kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji MO na kutoa ushauri wake kwa niaba ya kambi rasmi ya upinzani, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amejitokeza na kuunga mkono mapendekezo ya Lema.

Katika mkutano wake na wanahabari jana makao makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Lema alisema ni wazi kuwa Serikali inapaswa kuomba msaada kutoka vyombo vya kimataifa kama Scotland Yard na CIA katika kuchunguza tukio hilo kama kweli ina nia thabiti ya kumpata Bilionea huyo ambaye pia ni Mwekezaji kunako Klabu ya Soka ya Simba.

Katika chapisho lake alilolisambaa leo, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema kuwa pendekezo la Lema linapaswa kuchukuliwa kwa uzito unaostahili huku akitaka uchunguzi wa kutekwa kwa MO uwe na nguvu kubwa ili kuondoa taswira iliyoanza kujengeka nchini kuwa watu wanaweza kutekwa na hakuna kinachoweza kufanyika.

" Uchunguzi huru wa kimataifa utasaidia sana kurejesha imani ya raia na kuwaondolea hofu kuwa wakati wowote wanaweza kutekwa au hata kushambuliwa.

" Matukio ya kupotea kwa Afisa Utafiti na Sera wa CHADEMA Ben Saanane, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kibondo Simon Kanguye, Mwandishi wa Habari wa gazeti la Mwananchi Azory Gwanda na kushambuliwa kwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu yanadhihirisha kwa kiasi kikubwa sana vikwazo kadha wa kadha ambavyo polisi wetu wanakumbana navyo Katika Uchunguzi wa masuala kama haya ya jinai," amesema Zitto.

Zitto pia amehoji kitendo cha Polisi kushindwa kunasa namba za gari ambalo lilikuwa limebeba watekaji licha ya kwamba eneo hilo alilotekwa MO kuna zaidi ya 30 zazcamera za CCTV kuanzia Kanisa la Mt Petro huku pia makao makuu ya Idara ya Usalama wa Taifa yakiwa karibu na Hoteli hiyo.

" Haiwezekani kuwa mpaka leo ‘footages’ za camera hizi hazijachunguzwa na kupata Namba za gari zilizotumika kufanya utekaji huu na kisha kutambua umiliki wa gari hizi na kupata njia ya kumfikia MO alipo. Jeshi la Polisi linasema camera za hoteli ya collosium zilichezewa, watekaji hawawezi kuchezea camera za mtaa Mzima. Polisi wakipata msaada wa wenzao kutoka nje wanaweza kupata jawabu ya hili.

" Jambo lingine ni kuwa kuna kauli tata Kuhusu utekwaji wa Mohammed. Mwanzoni kabisa Polisi walisema kuwa MO alitii kukamatwa hakufanya harakati zozote. Hata hivyo ukweli umeanza kutoka kuwa MO alipambana. Katika kupambana alipiga kelele walinzi wasifungue geti la kutokea collosium Ndio maana watekaji wakapiga risasi Juu na kufungua geti wenyewe. Vile vile kiatu kimoja cha MO kilivuka na pia kofia ilivuka. MO Katika kuona anazidiwa alidondosha funguo ya Gari yake na simu ( naamini kuwa alidondosha funguo ya gari makusudi ili watu wachukue Gari kukimbiza watekaji). Bahati mbaya hapakuwa na mtu aliyethubutu kuwakimbiza watekaji wale. Kwanini hizi taarifa hazikutolewa kwenye press ya Mkuu wa Mkoa wa ZPC? Kwanini Umma uliambiwa kuwa MO alikubali tu kubebwa?

Zitto alisema kwenye mambo ya uchunguzi kuna suala la ganda la risasi ambayo ilitumika ambapo alihoji kama Polisi waliokota ambapo amesema kama lingepatikana lingesaidia kuweza kujua mmiliki wa silaha iliyotumika.

No comments :

Post a Comment