Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, November 17, 2018

Baada ya nyumba ya Kanye West kuungua kaja na hii isiyoshika moto!


Rapper Kanye West ‘Ye’ amekuja na mpango wa kujenga nyumba ambayo haitashika moto na hii ni baada ya tukio la nyumba yake yenye thamani zaidi ya shillingi Billioni 100 za Kitanzania kuwa miongoni mwa nyumba zilizoungua moto siku kadhaa zilizopita  Mjini California Marekani.

Moto huo mkubwa ulizuka na kuteketeza baadhi ya nyumba kwenye makazi ya kifahari ya Hidden Hills mjini California ikiwemo na nyumba nyingine kuteketea kabisa na  kusababisha vifo vya watu 71 mpaka sasa wakiwemo watu wa zima moto na kundi kubwa la watu kujikuta wakikosa makazi ya kuishi.

Kupitia ukurasa wa Twitter wa Kanye West ameandika “Najenga jamii ya kuzuia moto kushika”

Rapper Kanye West pamoja na mke wake Kim Kardashian waliajiri watu maalum wa uzimaji moto kwaajili ya kuzima moto uliosababisha uharibifu mkubwa wa nyumba za watu zaidi ya 27000 na maelfu ya watu kupotea.

No comments :

Post a Comment