dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, November 17, 2018

Hukumu kesi ya Tido Mhando, Des. 18!

HATIMA ya kesi ya Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando, dhidi ya tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh. milioni 887.1, itajulikana Desemba 18, mwaka huu, kama ana hatia au la.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya pande zote mbili kuwasilisha hoja za kama mshtakiwa ana hatia au la.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Leonard Swai, alidai kuwa upande wa Jamhuri umewasilisha hoja za majumuisho yao ya mwisho dhidi ya mshtakiwa.Wakili wa utetezi, Dk. Ramadhani Maleta, alidai kuwa wakili mwenzake Martin Matunda, amefariki dunia na wao pia wamewasilisha hoja zao za mwisho.

"Mheshimiwa tunaomba tarehe ya hukumu dhidi ya mshtakiwa kwa kuwa pande zote mbili tumewasilisha majumuisho yetu ya mwisho," alidai Swai.

Hakimu Shaidi alisema mahakama yake itasoma hukumu Desemba 18, mwaka huu na dhamana ya mshtakiwa inaendelea.

Oktoba 30, mwaka huu, upande wa utetezi ukiongozwa na mawakili (kwa siasa marehemu) Matunda na Dk. Maleta, walifunga ushahidi wa upande wao.

Upande wa Jamhuri uliita mashahidi wanne dhidi ya Mhando.

Miongoni mwa  mashahidi  wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi  katika kesi hiyo ni pamoja na  Ofisa Uchunguzi wa Takukuru, Victor Lesuya, Mwanasheria wa TBC, Gwakisa Mlawa na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC, Clement Mshana.

Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa Juni 16, 2008, akiwa  Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido ambaye alikuwa Mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.

Katika shtaka la pili, Tido anadaiwa kutumia vibaya madaraka yake Juni 20, 2008 aliposaini makubaliano kwa utangazaji wa digitali duniani kati ya TBC na BVl.

Katika shtaka la tatu, anadaiwa Agosti 11, 2008 na Septemba 2008 akiwa Dubai, Tido alitumia vibaya madaraka yake kusaini mkataba wa makubaliano kwa ununuzi, usambazaji kufunga vifaa vya usambazaji na mnara wa utangazaji kati ya TBC na BVI na kuifaidisha BVI.

Katika shtaka la nne, anadaiwa kuwa  Novemba 16, 2008 akiwa Dubai, Tido alitumia vibaya madaraka yake kusaini mkataba wa makubaliano kwa kuendesha miundombinu ya utangazaji (DTT Broadcast Infrastructure) kati ya TBC na BVI na kuinufaisha BVI.

Katika shtaka la mwisho,  anadaiwa kuwa kati ya Juni 16 na Novemba 16, 2008 akiwa UAE, Tido aliisababishia TBC hasara ya Sh.887,122,219.19.

No comments :

Post a Comment