Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amesitisha likizo za viongozi wote mkoani humo kutekeleza maazimio ya Jukwaa la Fursa za Biashara la mkoa huo.
Mwanri ameagiza kuwa, hata kama kuna likizo zimeidhinishwa zifutwe.
Amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo, Msalika Makungu kuandika barua kwa viongozi kuhusu uamuzi huo na amebainisha kuwa hakushauriwa na mtu, kaamua yeye.
Anayebisha anyooshe mkono, ajifanye angalau anajikuna tu; amesema Mwanri kwenye jukwaa hilo la nane lililomalizika leo.
Amewaeleza viongozi wa Tabora kuwa, mambo waliyopanga kuyafanya wakati wa likizo nje ya Tabora wanaweza kuyafanya mkoani humo hivyo wawaite ndugu zao waende mkoani humo.
Kiongozi huyo wa Tabora amewaagiza maofisa ugani mkoani humo watoke ofisini wahamie shambani.
Viongozi mbalimbali wamehudhuria jukwaa la Tabora akiwemo mwenyekiti wa jukwaa hilo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda, Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali, Hab Mkwizu na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora, Hassan Wakasuvi.
Viongozi wengine waliohudhuria jukwaa hilo ni wakuu wa wilaya, wakurugenzi watendaji wa Halmashauri, makatibu tawala wa wilaya, wenyeviti wa halmashauri za wilaya, wakuu wa taasisi na waendai wengine mkoani humo.

No comments :
Post a Comment