Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, November 22, 2018

RC Mwanri:Umasikini kwa wananchi wa Tabora haukuletwa na Mungu!


Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amesema, umasikini wa wananchi wa Tabora haukuletwa na Mungu, umesababishwa na wanadamu hivyo anataka Jukwaa la Fursa za Biashara liuwezeshe mkoa huo kunyonya maziwa.

Amesema, kabla ya kumalizika kwa jukwaa hilo kesho, halmashauri nane za mkoa huo na taasisi mbalimbali watasaini hati za makubaliano (MOU) na hatakubali Tabora ibaki kama ilivyokuwa.

Ameagiza kuwa, kila Halmashauri mkoani humo zioneshe miradi mitatu inayovutia wawekezaji na kwamba, Mkurugenzi atakayeshindwa kufanya hivyo hatoshi na ikifika Januari hatakuwa kwenye mkoa huo.

Mwanri amesema, halmashauri hizo za Kaliua, Uyui, Urambo, Igunga, Nzega Manispaa, Sikonge, Nzega Mji, na Manispaa ya Tabora zinapaswa kuonesha miradi, mipango na mipango mkakati ya kuitekeleza.

Anayekaa katika Halmashauri zetu ambaye hana mradi wa kutuonyesha hapa hatoshi, hatoshi, ataondoka tu, we nenda kachunge ng’ombe wako kama unataka nenda kafanye shughuli zako za nyumbani huko…” amesema.

Ameagiza watendaji mkoani Tabora kuacha urasimu na asiyetaka kubadilika aondeke, afunge mlango na aisahau Tabora.

Hatutakubali, hapa tunataka tupate badiliko la ghafla la kitabia, huo ndio msimamo wa mkoa;amesema na kuongeza kuwa baada ya jukwaa kazi hazitafanywa kwa mazoea.

Amewataka watendaji wawe na fikra za kiutu uzima na waache kufikiri kama watoto ambao kila kitu wakiambiwa wanasema nitamuambia daddy, nitamuambia daddy   

No comments :

Post a Comment