zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, November 24, 2018

Timu ya Mlandege yapigwa Faini kwa kosa la kufanya vurugu!


Chama cha soka Visiwani Zanzibar Kupitia Kamati ya Mashindano kimewapiga Faini Shilingi Milioni moja, laki mbili na hamsini elfu (1,250,000/=) Timu ya Mlandege Sports Club kwa kosa la kufanya vurugu na kuharibu mali kwenye mchezo wa ligi kuu soka Zanzibar Dhidi ya Timu ya maafande ya KVZ.

Mchezo huo ulipigwa katika Dimba la Cairo Kiwengwa ambapo mchezo ulimalizika kwa Timu ya Mlandege kufungwa bao moja kwa Bila.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Afisa Habari wa ZFA Abubakar Khatib (Kisandu) amesema baada ya kumalizika mchezo huo kati ya Mlendege dhidi ya KVZ baadhi ya Mashabiki wa Mlandege walifanya vurugu hadi kupelekea kutokea uharibifu mkubwa wa mali za watu na baadhi ya miundo mbinu ya uwanja huo.

Kisandu amesema baadhi ya mali ziliziharibiwa na mashabiki hao ni Gari aina ya Alphard, Gari iliyochukua Waamuzi (Nissan), vibendera vya uwanja na Geti la Mlango wa kutokea nje ambapo fedha hizo zinatakiwa kulipwa si zaidi ya tarehe 25/11/2018.

Adhabu hiyo imetolewa ZFA kwa mujibu wa kifungu (1-9) (1) (2) (3) (i) (ii) cha kanuni za ligi msimu wa mwaka 2018-2019.

No comments :

Post a Comment