
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema atafanya show nchini Kenya katika miji ya Mombasa na Nairobi kupitia tamasha lake la Wasafi Festival 2018.
“Tarehe 26 tutakuwa Mombasa katika Wasafi Festival, nakuja na niko vizuri Mombasa watafurahi sana. Tarehe 31 Disemba tutakuwa hapa Nairobi watu watafute tiketi mapema kwani najua watu watajaa sana," alisema Diamond."Kingine niishukuru sana My Government na Baraza langu la sanaa (BASATA) kwa kutupa nafasi hii tena, kutupatanisha na kufanya hizi show, kwa sababu inaonesha ni kiasi gani inasapoti muziki wa Tanzania inatupenda na inapenda tufanye vitu vilivyo bora.“
Diamond ameyasema hayo wakati akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Nairobi leo Desemba 21, 2018 Diamond huku akilishukuru Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kwa kuruhusiwa kufanya tamasha hilo nje ya nchi.
Mpaka sasa BASATA hilo hawajatoa taarifa rasmi kuhusiana na sakata hilo.
No comments :
Post a Comment