Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, December 21, 2018

MAPERA - GUAVAS!

Mapera ni matunda yanayo patikana kwa wingi lakini mara nyingi huwa hayapendelewi sana kutokana na ugumu wake wakati wa kuyatafuna pamoja na kuwa na mbegu mbegu nyingi. Hata hivyo matunda haya yana faida kubwa sana kwa afya ya mwili wa mwanadamu.

Zifuatazo ni faida kumi za mapera.

Utajiri wa Vitamin C.
Mapera yana utajiri mkubwa wa Vitamin C ambayo ni muhimu sana katika mwili wa mwanadamu.

Ni kinga nzuri ya kisukari.
Ulaji wa watu wengi unawaweka katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari lakini matumizi ya mapera yatakupunguzia hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari Hii ni kwa sababu mapera yana utajiri mkubwa sana wa Fibre.Fibre ni muhimu sana katika kupunguza kiasi cha sukari kwenye damu. Vilevile ni muhimu sana katika kuusafisha mfumo wa usahihi.

Kuimarisha Uwezo Wa Kuona.
Mapera yana utajiri mkubwa sana wa Vitamin A au Retinol ambayo ni muhimu sana katika kusaidia kuona vizuri.

Hivyo basi kama ilivyo kwa karoti, mapera yanasaidia sana katika kuongeza na kuimarisha uwezo wa mtu kuona.

Kurekebisha Kiwango Cha Shinikizo La Damu.
Madini ya Potassium yaliyomo ndani ya mapera yanasaidia katika ku-normalise shinikizo la damu ( Blood Pressure )

Ndizi na mapera vina kiwango cha potassium sawa.

Utajiri mkubwa wa Madini Ya Shaba
Mapera yana madini ya shaba ( Trace element copper ) ambayo ni mazuri sana katika ku- maintain ufanyaji kazi wa tezi ziitwazo thyroid.

Tezi za thyroid zisipo fanya kazi vizuri zinaweza kusababisha matatizo mengi ya kiafya kwa mwanadamu.

Utajiri wa Madini Ya Manganese
Mapera yana utajiri mkubwa wa madini ya manganese ambayo yanausaidia mwili katika kunyonya ama kupata virutubisho muhimu kutoka kwenye vyakula tunavyo kula.

Chakula tunacho tumia kikitumika vizuri mwilini, tunapata virutubisho vyote muhimu kama vile biotini, vitamin nakadhalika.
/Muungwana.

No comments :

Post a Comment