RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania.(UWT) Thuwaiba Editon Kisasa, kulia Katibu Mkuu wa UWT, Queen Mlozi na kushoto Mwenyekiti wa UWT Gaudensia Kabaka, walipofika Ikulu Zanzibar kumtambulisha Mwenyekiti wa UWT Taifa Kabaka.10-12-2018.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania,(UWT) Gaudensia Kabaka,alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar,akiwa na Ujumbe wake wa Viongozi wa UWT.kulia Makamu Mwenyekiti wa UWT Thuwaiba Editon Kisasa na Katibu Mkuu wa UWT. Queen Mlozi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ukiongozwa na Mwenyekiti wa Umoja huo Gaudensia Kabaka,Makamu Mwenyekiti wa UWT Thuwaiba Editon Kisasa na Katibu Mkuu wa UWT.B. Queen Mlozi, wakiwa katika ukumbi wa mkutona Ikulu leo wakati wa mazungumzo yao walipofika kujitambulisha.kwa Rais wa Zanzibar.(Picha na Ikulu)
Dk. Shein aliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na uongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, ulioongozwa na Mwenyekiti wa Umoja huo Gaudensia Kabaka ambao ulifika Ikulu kwa ajili ya kujitambulisha kwa Rais.
Rais Dk. Shein alisema kuwa bila ya akina mama mafanikio zaidi hayatofikiwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ndani ya (CCM) hasa ikizingatiwa kuwa wana umuhimu mkubwa katika jamii.
Alieleza kuwa kina mama ni vyema wakapewa nafasi katika kukitumikia chama chao na Serikali yao na ndio maana (CCM) ikaunda Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), ambao tokea kuasisiwa kwake umepata mafanikio makubwa na umekuwa muhimili muhimu wa (CCM).
Akitoa wito kwa Umoja huo, Rais Dk. Shein alisisitiza haja ya kuendeleza umoja, mapenzi na na mshikamano miongoni mwa Wanajumuiya sambama na kufanya kazi wakiwa wamoja.
No comments :
Post a Comment