Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, December 11, 2018

must, must read: THE FULL STORY OF SANI ABACHA'S RULE (1993 - 1998)!

TUNAJIFUNZA NINI KWA DIKTETA SANI ABACHA?
THE STRONGMAN ABACHA, DURING HIS HEYDAY!

November 17 mwaka 1993, aliyekuwa Mkuu wa majeshi wa Nigeria, Jenerali Sani Abacha, alijitangaza Rais wa nchi hiyo na kumpindua aliyekuwa Rais wa mpito Ernest Shonekan. Kabla ya mapinduzi hayo Shonekan alikuwa amekaa madarakani kwa miezi mitatu tu baada ya kujiuzulu kwa Jenerali Ibrahim Babangida.

Baada ya kuingia madarakani Abacha alianza kulalamika kuwa tawala zilizopita hasa ya Babangida iliharibu nchi na kuzorotesha maendeleo ya taifa hilo. Aliahidi kufufua njia kuu za uchumi, kujenga viwanda, kuboresha ufanisi katika sekta binafsi na na kuogeza wigo wa ajira kwa vijana.

Mara zote alilalamika kuwa nchi ilikuwa imeoza kwa kutafunwa na mafisadi katika serikali za awamu zilizopita. Alijipambanua kama kiongozi wanyonge na msema kweli. Alijitapa kuwa serikali yake itapunguza mikopo na misaada kutoka nje kwa kiasi kikubwa na kutumia rasilimali za ndani hasa mafuta kukuza uchumi.
Mwaka 1997 alijisifu kuwa amefanikiwa kuongeza akiba ya fedha za kigeni kutoka dola milioni 494 hadi dola bilioni 9.6 kwa miaka minne aliyokaa madarani. Pia alitangaza kuwa amepunguza deni la nje kutoka dola Bilioni 36 hadi Dola Bilioni 27.

Lakini pamoja na kujisifu kwa maendeleo ya kiuchumi, aliongoza Nigeria kwa mkono wa chuma. Alishutumiwa kuvunja haki za binadamu, kukiuka misingi ya demokrasia na utawala bora na kutishia uhuru wa vyombo vya habari.

Alijipa mamalaka isiyohojiwa na chombo chochote cha sheria nchini humo. Alipiga marufuku shughuli za kisiasa na kuwafunga 
 jela waliomkosoa. Wanaharakati wengi waliuawa, wengine kufungwa jela na wengine kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Miongoni mwa wanasiasa waliosota jela wakati wa utawala wa Abacha ni Rais wa zamani wa taifa hilo Jenerali Olusegun Obasanjo aliyeshtakiwa kwa uhaini.

Abacha hakuishia kwa wanasiasa tu, alishughulika na yeyote aliyekosoa utawala wake hata kama ni kwa nia njema. Aliagiza kunyongwa kwa mwanaharakati wa mazingira kutoka jamii ya Ogoni, Ken Saro-Wiwa, baada ya kuanzisha kampeni ya kupinga uharibifu wa mazingira uliokuwa ukifanywa na makampuni ya kuchimba mafuta kwenye eneo lao.

Saro-Wiwa aliuawa November 10 mwaka 1993 kwa agizo la dikteta Abacha. Mauji yake yalichochea hasira kutoka mataifa mbalimbali na kusabisha Nigeria kufutiwa uanachama wa Commonwealth kwa miaka mitatu.

Si hao tu, Abacha alinyanyasa wafanyabiashara wakubwa, na kuwapa kesi za uhaini, uhujumu uchumi na utakatishaji wa pesa ili aweze kuwashughulikia vizuri. Mmoja wa wafanyabiashara walioingia kwenye '18' zake ni  Moshood Abiola aliyekuwa tajiri nambari moja Afrika kwa wakati huo (akiwa na utajiri wa dola Bilioni 5 (shilingi Trilioni 12 za kitanzania).

Abiola alikamatwa kwa kesi ya uhaini akidaiwa kujitangaza Rais ‘halali’ wa Nigeria. Hii ni kwa sababu mwaka 1993 Rais Ibrahim Babangida aliitisha uchaguzi mkuu, ambapo Abiola aligombea na kudaiwa kushinda, lakini Babangida akafuta matokeo ya uchaguzi (kama alivyofanya Jecha), na kumteua Ernest Shonekan kuwa Rais wa mpito wa Nigeria.

Abiola hakukubali kuporwa haki yake ya ushindi, akaenda kuomba support kwenye jumuiya za kimataifa. Lakini wakati akiwa huko, ndipo Jenerali Sani Abacha akampindua Rais wa mpito (Shonekan) na kujitangaza Rais. Kwahiyo Abiola alikuta Shonekan ameshapinduliwa na Abacha ndiye Rais. Alipohoji haki yake ya ushindi kwenye uchaguzi mkuu uliopita, alikamatwa na kuwekwa jela kwa madai ya uhaini.

Dikteta Sani Abacha hakuishia hapo, alimuua mke wa Abiola (Bi.Kudirat Abiola) mwaka 1993 baada ya mkewe huyo kutaka mumewe aachiwe huru na kufutiwa mashtaka yaliyokua yakimkabili.

Baada ya kelele nyingi za kimataifa za kutaka Abiola aachiwe huru, Dikteta Sani Abacha aliagiza Abiola aachiwe July 7 mwaka 1998, lakini apewe mateso makali kabla ya kuachiwa. Inadaiwa alipigwa kiupigo kikali na kusababisha kufariki kabla ya kuachiwa huru.

Serikali haikutaja sababu za kifo chake lakini ndugu zake walidai alikufa kwa kipigo. Aliyekuwa Afisa Usalama wa Jenerali Abacha, aitwaye Hamza Al-Mustapha alidai kuwa anayo video ya siri iliyorekodiwa wakati Abiola akipigwa hadi kukata roho gerezani. Alidai kuwa yeye kama mshauri wa usalama wa Abacha, alimshauri asimuue Abiola lakini alikaidi ushauri huu.

Mkono wa chuma wa dikteta Sani Abacha haukuishia kwa wanasiasa na matajiri tu, ulikwenda hadi kwa waandishi wa habari, waandishi wa Makala na vitabu. Mwanafasihi mkongwe na mwenye heshima kubwa barani Afrika, ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Nobel, Wole Soyinka aliponea chupuchupu kuuawa na serikali ya Abacha mwaka 1997.

November 16 mwaka huo, Dikteta Abacha alitangaza Wole Soyinka akamatwe, lakini alitoroka kwa baiskeli kwa kupitia njia za ‘panya’ hadi Benin, ambapo alipanda ndege kwenda Marekani na kupata hifadhi ya kisiasa. Hata hivyo Abacha alisaini hati ya adhabu ya kifo kwa Wole Soyinka licha ya kutokuwepo Nigeria.

Mwezi mmoja kabla ya Abiola hajauawa, Dikteta Sani Abacha alikufa ghafla kwenye Ikulu yake mjini Abuja. Taarifa ya serikali ilieleza kwamba Abacha alikufa kwa shambulio la moyo, lakini ripoti ya uchunguzi ya gazeti la New York Times iliyochapwa July 11, mwaka 1998 ilieleza kuwa Abacha aliuawa kwa sumu na makahaba aliokuwa amewakodi kutoka Dubai ili kwenda kumburudisha.

Usiku wa tarehe 8 June, Abacha alikesha na makahaba hao wawili wakilewa, kuogelea na kucheza mziki katika Ikulu ya nchi hiyo. Majira ya saa 10 alfajiri Abacha alidai kutojisikia vizuri na kwenda kupumzika, na ilipofika saa 12 asubuhi alifariki dunia.

Baada ya kifo chake madai mbalimbali ya ubadhirifu wa mali na matumizi mabaya ya fedha yalibainika. Ilibainika kwamba licha ya Abacha kulalamikia matajiri kuhujumu rasilimali za taifa hilo, na kujifanya yeye ni Rais wa wanyonge, lakini alitumia nafasi yake kujilimbikizia mali na kufilisi nchi. Familia ya Abacha ilikutwa na dola Bilioni 5 (karibu trilioni 12 za kitanzania) zikiwa kwenye akaunti mbalimbali nje ya nchi hasa Ulaya na Marekani.

Abacha pia anadaiwa kufanya 'cash transaction' kutoka benki kuu ya Nigeria na kuzitumia kwa matumizi yake mbalimbali alipokuwa Ikulu. Alizitumia kugawia wananchi na kutoa zawadi. ilikuwa desturi yake kutembea na ‘maburungutu’ ya fedha kwenye ziara zake mbalimbali. Utaratibu huu wa kuchukua fedha taslimu (cash) na kuzitumia kiholela, uliingizia benki kuu ya Nigeria hasara ya Dola Bilioni 1.4 (karibu shilingi trilioni 3 za kitanzania).

Taarifa ya uchunguzi wa kimataifa ilionesha pia kuwa jina la Abacha lilitumika mara 419 kuidhinisha malipo na kuchukua pesa kutoka makampuni makubwa nchini humo kwa ajili ya familia yake. Ndugu zake walipotaka fedha aliwaandikia 'memo' kwenda benki kuu au kwenye makampuni makubwa ya kuchimba mafuta na kupewa kiasi walichotaka.

Licha ya ubadhirifu wote huo, Abacha alikua akilalamika kuwa nchi hiyo ilifilisiwa na mafisadi waliokuwa wakilindwa na tawala zilizotangulia. Waliomkosoa Abacha waliitwa vibaraka wanaotumiwa na mabepari.

Mwaka 2014 serikali ya Marekani ilikubali kurudisha dola milioni 480 (karibu shilingi trilioni 1 za kitanzania) kwa serikali ya Nigeria, fedha ambazo zilikuwa zimefichwa nchini humo na serikali ya Abacha. Mwaka huohuo, serikali ya Liechtenstein ilikubali kurudisha dola milioni 227 kwa serikali ya Nigeria, zilizokua zimefichwa visiwani humo na familia ya Abacha.

Umejifunza nini?

Makala kwa hisani ya Malisa GJ. 
Ni SamuNgwegwe. Asante


No comments :

Post a Comment