Chama cha Conservative kimefikia maamuzi ya kupiga kura kuhusu kumuamini au kutomuamini Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May.Hilo ni pigo kubwa kwa Theresa May ambaye ameonekana kugeukwa na chama chake mwenyewe.
Waziri Mkuu huyo wa Uingereza,aliahirisha kuidhinishwa kwa mkataba wa Umoja wa Ulaya (EU) katika bunge.
Chama hicho kimekaa chini na kuamua kupiga kura kuutizama uongozi wa Theresa May kama unaaminiwa ama la.
Wanachama wanataka waziri huyo apate angalau asilimia kumi na tano ya kura zote.
Waziri wa haki David Gauke amesema kuwa Theresa May atapashwa kuahirisha kujitoa kwa Uingereza Umoja wa Ulaya endapo uongozi wake hautapigiwa kura za kutosha.
"Sidhani kama tutaondoka EU tarehe 29 Machi." alisema Gruke.
No comments :
Post a Comment