Msemaji wa serikali na waziri wa mawasiliano wa Gabon afahamisha kukamatwa kwa wanajeshi waliojaribu kupindua serikali.
Guy-Bertrand Mapangou, waziri wa mawasiliano na msemaji wa ikulu wa Gabon afahamisha kwamba wanajeshi waliojaribu kupindua serikali na kutangaza katika kituo cha taifa cha redio wametiwa mbaron.
Waziri huyo wa mawasiliano wa Gabon ameyasema hayo katika kituo kimajo cha habari cha Ufaransa kwa kuthibitisha kuwa wanajeshi hao wametiwa mbaroni na kikosi cha GIGN baada ya kuendesha operesheni ya kuokoa kituo cha redio cha taifa kilichokuwa kimetekwa na wanajeshi hao waliotajwa kuwa wameasi mapema Jumatatu.
Hali imerejea kuwa shwari baada ya muda mchache baada ya makabiliano alifahamisha waziri wa mawasiliano.
Wanajeshi walioasi walitangaza katika kituo cha redio cha taifa kuwa wanataraji kulifanyia marekebisho baraza la kitaifa.
Tangazo lililosomwa na Ondo Obiang Kelly liligonga vichwa vya habari katika vyombo vya habari huku na kule ulimwenguni.
Jarida la Gabonactu limesema kuwa kulisikika milio ya risasi mjini Libreville karibu na kituo cha redio ya taifa.
Taarifa zinafahamisha kuwa muda mchache baada ya wanajeshi walioasi kutangaza kupindua serikali , kituo hicho cha redio kilipoteza mawasiliano na mitandao ya kijamii kufungwa.
Habari kutoka ikulu zinasema kuwa maeneo yote ya kimkakati nchini Gabon yapo chini ya milki ya serikali.
Ikumbukwe kuwa rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba alipatwa na maradhi ya khafla akiwa nchini Saudia Oktoba 24 na kusafirishwa nchini Morocco Novemba 28.

No comments :
Post a Comment