Mashirika ya wafanyakazi, makundi ya wapinzani kwa ushirikiano nchini Sudan watoa wito wa maandamano.Katika taarifa iliotolewa na viongpozi wa wapinzani na mshirika ya wafanyakazi imefahamisha kuwa maandamano yatafanyika katika miji tofauti nchini Sudan Jumanne.
Maandamano ya kupinga kupanda kwa bei za bidhaa mahitaji katika jamii. Maandamano hayo yanafanyika nchini Sudan tangu Disemba 19.
Maandamano hayo yalibadilisha sura yake na kuwa maandamano ya kupinga serikali ya rais Omar Al Bashir na kumtaka kuondoka madarakati.
Jeshi la Polisi lilitumia mabomu ya kusabisha kutokwa na machazo kuwatawanya waandamanaji.
Shirika la Amnesty International limesema kuwa watu 40 ndio waliofariki kufuatia maandamano hayo nchini Sudan.
No comments :
Post a Comment