Na.Thabit Madai, Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mahamoud amewataka jumuiya ya wazazi Chama cha Mapinduzi kuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha wanawalea vizuri vijana na kuwa katika maadili yaliyokuwa mema.
Akifungua mkutano wa mwaka wa baraza kuu la wazazi wilaya ya dimani kichama amesema kufanya hivyo kutawezesha vijana kuwa na heshima na taifa kuwa na nguvu kazi
Amefahamisha hatua hiyo pia itaweza kuwa na vijana wazazlendo na wenye kujitambua ili kukiwezesha chama cha mapinduzi kuwa imara na kushinda katika chaguzi mbali mbali za chama hicho na uchaguzi mkuu ifikapo mwaka 2020.
Amesema chama cha mapinduzi ni chama chenye sera zinazokubalika, hivyo ni vyema wazazi, vijana na wananchi wote kwa ujumla kuhakikisha wanakilinda chama chao ili kuona maendeleo yanapatikana hapa nchini.
Aidha mhe ayoub amesema serikali itaendelea kupambana na vitendo vya udhalilishaji vinavyojitokea katika maeneo mbali hatimaye vinaondoka kabisa.
Nae katibu wa jumuiya ya wazazi wilaya ya dimani kichama bw makame ameir yussuf akitoa taarifa ya mpango kazi ya baraza hilo amesema jumuiya hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanapambaana na vitendo vya udhalilishaji na kuwafunza maadili mema vijana wa wilayahiyo.
Hivyo amewaomba wazazi kuwasimamia watoto wao kimalezi kwa lengo la kuwa na vijana wachapakazi na kutunza mila na silka za kizanzibar.

No comments :
Post a Comment