Kwa kutambua umuhimu wa michezo kwa maendeleo ya Zanzibar Awamu zote Saba za uongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimefanya jitihada mbali mbali za kuimarisha sekta ya michezo ikiwemo miundombinu ya michezo hasa ujenzi wa viwanja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein ameyasema hayo leo huko katika uwanja wa Gombani Pemba mara baada ya kushiriki kikamilifu katika Bonanza maalum la Mazoezi ya Viungo ambalo lilianzia Wawi Matrekta hadi uwanja wa Gombani Chake Chake Pemba.
Mazoezi hayo ya viungo yalivishirikisha vikundi mbali mbali vya mazoezi kutoka Unguja, Tanzania Bara pamoja na wenyewe kutoka Pemba ambapo pia, yaliwashirikisha viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na Serikali akiwemo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd pamoja na wananchi.
Katika hotuba yake aliyoitoa mara baada ya mazoezi hayo ambayo hufanyika Kitaifa kila mwaka mnamo tarehe mosi ya mwezi wa Januari, Dk. Shein alisema kuwa katika Awamu ya mwanzo ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume ulijengwa uwanja wa Amaan ambao ni wa kisasa wenye viwango vya Kimataifa uliofunguliwa rasmi mwaka 1970.
Aidha, katika Awamu ya Nne Marehemu Sheikh Idriss Abdulwakil alianzisha ujenzi wa uwanja wa Gombani Pemba.
Katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2015-2020, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba imefanya jitihada kubwa za kuimarisha miundombinu ya michezo ikiwa ni pamoja na kukifanyia matengenezo na kukiwekea majani ya bandia na mpira wa kukimbilia kiwanja cha Amaan na Gombani.
Vile Vile, Rais Dk. Shein alisema kuwa kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kimejengwa upya kiwanja cha michezo cha Mao Tse Tung ambacho kinaweza kutumika kwa michezo mbali mbali .
Kwa maelezo ya Rais Dk. Shein kiwanja hicho kinaweza kutumika kwa michezo ya mpira wa mikono, mpira wa wavu, mpira wa vikapu, mpira wa pete na mpira wa miguu hatua ambayo itaondokana na tatizo la uhaba wa viwanja vya michezo na kusaidia kuimarisha sekta ya michezo.

No comments :
Post a Comment