Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, March 16, 2019

Hatma ya Maalim Seif CUF kujulikana kesho (leo)!


Kesho Jumamosi Machi 16, 2019 Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) kuitisha mkutano ili kujadili jina la mrithi wa nafasi ya Katibu Mkuu.

Mwenyekiti atateua majina matatu kwa kushauriana na makamu wenyekiti wa chama hicho Bara na Zanzibar kisha majina yatawasilishwa kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi na kuchagua jina moja hiyo ni kulingana na mabadiliko ya katiba ya chama hicho.

Mkurugenzi wa Habari wa CUF Abdul Kambaya amesema uchaguzi wa kanda umekamilika mapema leo watajulikana wajumbe wa Baraza Kuu ambao watafanya mkutano wao wa kwanza kesho.

"Hivi tunavyozungumza nipo kwenye kikao, viongozi wakuu nao wana kikao kabla ya kuitisha kikao cha Baraza Kuu la Uongozi hapo kesho kujadili majina yatakayowasilishwa na Mwenyekiti ili kumpata Katibu Mkuu wa chama," amesema Kambaya.

Kambaya amefafanua kuwa leo na kesho hakutakuwa na taarifa yoyote hadi vikao hivyo vimalizike.

Hatua hiyo ya CUF imekuja baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa kanda ambao umefanyika kwa siku tatu juzi jioni, jana na leo Ijumaa ili kupata wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi.

No comments :

Post a Comment