Wabunge 321 wamepiga kura kuipinga hatua hiyo huku 278 wakiunga mkono Uingereza kuondoka kwenye umoja huo kiholela, Kura ya jana imepigwa baada ya ile ya Jumanne, ambapo wabunge waliukataa mpango wa Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May kuhusu masharti ya nchi hiyo kuachana na Umoja wa Ulaya, maarufu kama Brexit.
Hatua ya Uingereza kuondoka bila ya makubaliano kuhusu uhusiano wa baadae kati ya pande hizo mbili, ingesababisha hatari kubwa katika biashara na mustakabali wa watu wa Uingereza na Umoja wa Ulaya.

No comments :
Post a Comment