"Asanteni sana kwa ku-share ujumbe wa yule mhitaji wa Singida mwenye kidonda mgongoni.
Hatimaye nimefanikiwa kumpata huyu dada, anaitwa Mariam Rajab (25), anatokea
Singida Mjini, Mtaa wa Minga, Kata ya Mnung'una.
Atasafirishwa kesho kuja DSM kwa ajili ya kuanza matibabu Muhimbili.
Kwa wale walionijia inbox ili kutaka kumsaidia ningeshauri tusubiri kwanza aletwe Dar ndipo hayo yafuate,lakini sisi kama hospitali kwa upande wetu tutamtibu bure.
Asante kwa Msaada wenu.
Ni Mimi,
Aminiel Aligaesha
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano,
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
0786 648636
16.04.2019"
No comments :
Post a Comment