AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, April 4, 2019

Spika Ndugai: Bunge limeazimia kutofanya kazi na Profesa Mussa Assad si ofisi ya CAG. Ripoti itasomwa endapo haijasainiwa na Prof. Assad!

spika-jpg.1062521
Spika wa Bunge, Job Ndugai ametoa ufafanuzi juu ya azimio la Bunge la kutokufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuwa Bunge limeazimia kutofanya kazi na kutoshirikiana na CAG na sio ofisi ya CAG. Kwa mantiki hiyo, ripoti itasomwa endapo haijasainiwa na ASSAD. 

Dodoma. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema Bunge lilitangaza kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad na si ofisi yake.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo mchana Alhamisi Aprili 4, 2019 baada ya kuwatambulisha wageni walioalikwa bungeni, akiweka sawa hali ya sintofahamu iliyoibuka baada ya Bunge kutangaza kutofanya kazi na Profesa Assad.
“Hakuna wakati wowote ambao Bunge limekataa kufanya kazi na taasisi ambayo ni ofisi ya CAG. Bunge hili limekataa kufanya kazi na mtu anayeitwa Profesa Assad basi. Tusiripoti tofauti tukauchonganisha umma na kuuchanganya,” amesema Ndugai.

Aprili 2, 2019 Bunge lilipitisha azimio la kutofanya kazi na Profesa Assad kwa sababu ya kauli yake aliyoitoa wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kuwa Bunge ni dhaifu.


/ Mwananchi


No comments :

Post a Comment