Ikulu ya Marekani imebainisha kwamba Rais Donald Trump alizungumza kwa simu na mbabe wa kivita wa Libya, Jenerali Khalifa Haftar, akimuahidi kumuunga mkono. Hayo ni licha ya kuwepo kwa jitihada za Umoja wa Mataifa kusitisha mapigano kati ya jeshi la serikali inayotambuliwa kimataifa na wapiganaji wa Jenerali Haftar.
Katika mazungumzo hayo ya jana, Trump na Haftar walijadiliana hatua za kupambana na ugaidi na haja ya kufikia amani na utangamano nchini Libya, kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani. Taarifa ya Ikulu hiyo inasema kwamba Trump alilitambuwa jukumu muhimu la Jenerali Haftar katika kupambana na ugaidi na kulinda rasilimali ya mafuta ya Libya.
Wachambuzi wanasema sasa Marekani imeungana rasmi na Misri na Umoja wa Falme za Kiarabu katika kumuunga mkono mbabe huyo wa kivita, ambaye ametangaza rasmi kutaka kuutwaa mji mkuu, Tripoli, unaodhibitiwa na serikali inayoongozwa na Waziri Mkuu Fayez al-Sarraj, anayetambuliwa na Umoja wa Mataifa.

No comments :
Post a Comment