Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, July 30, 2019

Balozi Amina awataka wajasiriamiali kuchangamikia maonesho ya SADC!

WAZIRI wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali amewataka Wajasiriamali wa Zanzibar uchangamkia  fursa ya maonyesho ya SADC ya wiki ya viwanda inayotarajiwa  kufanyika katika hivi karibuni katika ukumbi wa Mwalim Nyerere Dar es  Salaam

Akizungumza na waandishi wa habari   ofisini kwake Migombani, Unguja Balozi Amina  alielezea kuwa Wajasiriamali wanatakiwa kuchangamkia fursa hiyo kwa kuonesha bushes ambazo wanazitengeneza.

Aliongeza kuwa umuhimu wa kushiriki kwa wawekezaji wa viwanda , wajasiriamali wa Zanzibar na  jinsi watavyojitangaza kupitia mkutano huo ambao utaanza tarehe 4-9 mwezi ujao.
"Wajasiriamali wa Zanzibar wanaweza kushiriki katika wiki ya viwanda kwa kutangaza bidhaa zao ambazo zina viwango kwa lengo la kujulikana kupitia maonesho halo" alisema balozi Amina Salum Ali.

Aidha alisema Zanzibar tuna fursa nyingi kwa upande wa SADC na kuwataka wafanyabiashara, wajasiriamali kutoa bidhaa zinazokuwa na mvuto ikiwemo mwani, vanilla, mafuta ya karafuu, mafuta ya nazi  na baadhi ya bidhaa nyengine adhimu za Zanzibar.

“Tuacheni woga tutangaze biashara zetu , wajasiriamali waonyeshe mambo ya kizanzibar yenye mvuto yakiwemo ya Utalii, Spice za kila aina tulizonazo hapa Zanzibar”, alifahamisha Waziri Amina.

Akitoa wito kwa wafanyabiashara kutumia fursa ya kufanya mambo mengi katika wiki hiyo ambayo yatasaidia kutangaza  biashara na milango iko wazi ya kuendeleza sekta ya biashara nchini .

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda  Juma Hassan Reli alisema SADC ni jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika ambao umoja wake umeundwa kwa kurahisisha wafanyaji biashara na kuweka vigezo mbali mbali vya kuichumi.

Alisema wafanyaji biashara wawe na  uwiano wa kodi ili kuweza kusababisha umoja wa  soko na uchumi kwa kuweza kubadilishana uzoefu na kuingiza kipato.

Alisema wageni wanaokuja ni viongozi wakuu wakiwemo mawaziri makatibu na marais na hii ni nafasi pekee  ya kujitangaza kupitia wageni hao kwa kununua bidhaa zao.

 Pia alisema kwa upande wa Zanzibar tumepata mabanda kumi kwa lengo la kuonesha bidhaa  mbali mbali zenye kiwango zilizothibitishwa na ZBS hivyo waichangamkie nafasi hiyo ambayo mwaka huu inafanyika Tanzania.

Alisema wageni wataoshiriki tayari wameshaandaliwa mambo yote muhimu ikiwemo usafi kusafishwa sehemu zote ili kunusurika na maradhi mbali mbali na pia wageni hao wanatarajiwa kutembelea hadi Zanzibar kuona vivutio mbali mbali vya utalii.

Vile  vile aliwataka wajasiriamali wajitokeze kwa wingi kupitia chamber commercial kwani faida nyingi zitapatikana ikiwemo fursa ya ajira.

Nao  wafanya biashara walisema wamefarijika kufanyika maonesho ya wiki ya viwanda Tanzania kwani wataweza kujitangaza na kupata utaalamu, kubadilishana mawazo  na kujenga uhusiano na wafanyabiashara  na wajasiriamali wenzao kutoka nchi mbai mbali.

No comments :

Post a Comment