Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, July 31, 2019

Bodi mpya ya Ushauri Ofisi ya mkugazi mkuu wa elimu washauriwa kufanya kazi kwa kufuata Sheria!

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar na Riziki Pembe Juma ameitaka bodi mpya ya Ushauri ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Elimu, kufanya Kazi kwa kufuata Sheria za Bodi hiyo ili kuleta maendeleo katika Elimu.

Amesema sheria zimewekwa kwa malengo ya kuongoza na kutenda haki, hivyo ni vyema kuitumia kwa kuleta mafanikio na kuacha muhali katika kutenda haki.

Akizungumza wakati alipozindua bodi hiyo katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Mazizini Mjini Unguja, Mhe Riziki amesema maamuzi wanayoyatatua ni lazima kuyafikisha kwake ili kuyapitisha na endapo yatakuwa ni mazito yaweze kufikishwa Serikalini.
Aidha amewataka kuwafuatilia vyema walimu kwani baadhi yao wamekuwa wakikwepa baadhi ya vipindi vyao kwa kuchelewa kazini au kutika mapema, na hivyo kusababaisha kutomaliza silabasi zao kwa wakati na kupelekea kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.

Hivyo amewataka kutokuwa na muhali juu ya walimu kama hao kwa kuwachukulia hatua za kisheria kama inavyoelekeza kwa kuwawajibisha Pasi na kufanya uonevu wa aina yeyote ili kuleta maendeleo katika sekta ya Elimu nchini.

Pia amewataka kushirikiana na kuweka mbele uzalendo wa nchi yao pamoja na kudhibiti siri za vikao vyao pamoja na kuisaidia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar ili kupiga hatua katika maendeleo ya Elimu nchini.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Elimu Dkt Ali Makame Ussi amesema Taifa linahitaji kuwa na mfumo madhubuti na unaoleta tija katika kusimamia na kuendeleza Elimu, na ndio maana kukawekwa miongozo maalum ya sheria, kanuni, pamoja na Sera ili kufikia malengo hayo.

Amesema kuundwa kwa bodi hiyo kutatoa nafasi ya kusimamia majukumu ya Elimu na kuendeleza miongozo hiyo ili kufikia malengo ya kusimamia muelekeo wa Serikali katika kutoa Elimu bora kwa jamii nchini.

Hivyo amesema kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha suala la maendeleo hayo yanafikiwa kwa kuwepo mashirikiano ya pamoja katika idara zote za Elimu.

Bodi ya Ushauri ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Elimu imeundwa ikiwa na wajumbe saba chini ya Mwenyekiti wake Dkt Ali Makame Ussi, ambayo itafanya kazi zake kwa muda wa miaka mitatu.

No comments :

Post a Comment