Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, July 30, 2019

Watu 65 wauwawa Nigeria!

Televisheni ya taifa nchini Nigeria imeripoti jana Jumapili kuwa takriban watu 65 wameuwawa wakati washambuliaji wanaoaminika kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la Boko Haram walipovamia shughuli ya mazishi kaskazini mashariki ya Nigeria.

Afisa wa serikali ya eneo hilo, Mohammed Bulama amesema, hapo kabla watu 21 waliuwawa wakati wa mazishi kwenye kijiji cha Badu katika jimbo la Borno na wengine 44 waliuwawa baadaye wakati walipofika katika eneo la tukio kujaribu kuwaokoa wale walikuwa wakishambuliwa.


Wakati wa tukio hilo washambuliaji 10 pia waliuwawa. Kundi la Boko Haram limekuwa kitisho kwa wakaazi wa kaskazini mashariki ya Nigeria na limekuwa likifanya mashambulizi katika nchi jirani za Chad, Niger na Cameroon.

Tangu mwaka 2009, makumi kwa maelfu ya watu wamekufa na inakadiriwa wengine milioni 2.5 wameyahama maakazi yao kutokana na ukatili unaoendeshwa kundi hilo la wapiganaji wa itikadi kali.

No comments :

Post a Comment