CHAKUFANYA SIKU YA ARAFA  
1) lala mapema usiku wake2) amka saa kumi na robo za alfajiri
*3)*swali rakaa 2 tahajjud na rakaa moja witri na uombe wakati wa sijda
4) baadae fanya istighfaar mpaka karibu na swala ya fajri
5) Jiandae na swala ya fajri ikiwezekna tawadha tena ili umwage dhambi kwa maji ya udhuu
6) Soma dua baada ya kutawadha
7) swali rakaa 2 kabla ya fajri kwani mtume swalla Allahu aleyhi wassalam asema hizo ni bora kuliko dunia na zilioko ndani ya dunia
Swali fajri na ubaki kwenye mswala mpaka usome dua z asubuhi alafu soma quran mpaka jua lichomoze
8) ikifika 6:35 am swali rakaa 2 za " ishraaq" ili upate thawabu za Hajj na Umrah
10) lala kidogo angalau kwa jisaa moja ili upate afiya ya kufanya ibada nyengine
Ukiamka tawadha na uswali rakaa 2 za dhuha
11) endelea kufanya dhikri , istighfaar na kusoma Qur'an
12) soma sana hii: لا اله الا الله وحده لاشريك له ,له الملك وله الحمد وهو علي كل شيء قدير
13) swali dhuhri soma quran kidogo
14) swali asri soma adhkaar za jioni
15) soma quran kabla ya adhaan ya maghrib na endelea kuomba dua na usiwasahau waislamu wenzio kwa dua
16) muombe Allah jua la siku ya Arafah lisizame ila umeachwa huru na moto
17) ikiadhiniwa maghrib futuru na usisahau dua kwa wingi kwani dua ya anaefunga hazirudishwi
Ukiweza kuyafanya haya kwa masiku yote tisa ni bora zaidi maana thawabu zake ni nyingi mno!!!
وبا الله التوفيق
https://lifeinsaudiarabia.net/blog/2017/08/24/5-virtues-of-the-day-of-arafah-every-muslim-should-know/
 
 
 
 
 
 
No comments :
Post a Comment