dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, August 27, 2019

Ijue Hoteli ya kifahari iliyojengwa kwenye shimo lenye kina cha mita 88!


Hoteli ya Intercontinental Shanghai Wonderland pia maarufu kwa jina Shimao Quarry Hotel inapatikana katika wilaya ya Songjiang jijini Shanghai, China ya mashariki. Hoteli hiyo imejengwa kwenye shimo kubwa lililotokea kufuatia miaka nyingi ya uchimbaji wa changarawe kwa ajili ya ujenzi wa barabara..

Hoteli hii ambayo ilifunguliwa mwaka jana (2018) iko na orofa 18 kwa jumla; orofa mbili zikiwa chini ya maji na mbili pekee zikiwa zinaonekana ukiwa juu ya ardhi. Hoteli hii yenye vyumba 336 iko na mgahawa wa kifahari, sehemu ya michezo na burudani za aina mbalimbali.

Hoteli ya Intercontinental Shanghai Wonderland ni kivutio kikuu cha watalii kwa sababu ya ujenzi wake wa kustaajabisha na pia vyumba vyake vyenye maandhari ya kipekee.

No comments :

Post a Comment