Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, August 31, 2019

KUKAMATWA KWA NDEGE: KIJANA MACHACHARI ABDUL NONDO NAE AJA NA YAKE MAPYA!

Kwanini Prof. Kabudi na AG wasishtakiwe kwa kuingiza Taifa letu hasara? - Auliza Abdul Nondo!
Above: Kijana machachari Abdul Nondo ambae aliwahi kutekwa, asisitiza kuwa Prof. Kabudi inafaa ashitakiwe kwa kulitia Taifa hasara!

By Abdul Nondo.
Tumekuwa tunadanganywa danganywa kwa kisingizio cha taifa letu ni huru na mambo ya uzalendo huku watu waliopewa mamlaka kumshauri Mh.Rais ,wanashindwa kufanya hivyo kikamilifu.

Leo nilipo alikwa Star Tv tuongee Asubuhi na Aloyce Nyanda na Kamoti ,nilielezea vyema kabisa ila kwa faida ya wengine na Taifa letu naomba nirudie kuweka mlolongo wa kesi hii hadi ndege yetu kukamatwa.

Ipo hivi.

Mwaka 1983 , Serikali yetu ya Tanzania ilitaifisha mali za Hermunus Philippus Steyn ,kukawa na majadiliano ya kumlipa fidia ya muda mrefu, ilipofika tar 8,Novemba 1993 ,Serikali ya Mwinyi ikakubali kumlipa fidia taratibu taratibu.
Ila malipo yakawa yanasua sua ,mwaka 2010 akafungua kesi ya arbitration  (Mahakama ya usuluhishi Dar) chini ya Jaji Josephat Mackanja  ndani nchini Tanzania ,Dar .Steyn akashinda , Mahakama ilia amuru alipwe USD Mil .36 ,ila serikali ikajadiliana nae kupunguza akakubali kupunguza hadi USD milion 30.

Makubaliano hayo yalipewa nguvu kama hukumu ya kimahakama  kuu ,tar 3/05/2011 (it was registered as the judgement of the court /Court degree for being executed) chini ya Jaji Makaramba  ndani ya Dar ,Tanzania.

Serikali ilikuwa inalipa taratibu deni lile USD Mil.30.Hadi kufikia tarehe 3/Machi/2016 serikali ilikuwa tayari imelipa USD mil.20 (USD mil.20,099,155.12) ilikuwa kama kiasi cha USD Mil.9 tumalize deni.

Tarehe 17/Julai/2018 ,Kwa ushauri wa Prof.Kabudi na Mwanasheria mkuu wa Serikali, serikali yetu ikafungua kesi No.168 ya 2018 Mahakama kuu chini ya Jaji Phillip, wakiomba Mahakama iwape ruhusa ya ku- review ,au kupitia upya tena maamuzi  yale ya 2010 ya kumlipa bwana Steyn ,kwasababu sababu yalikosewa ,pia fidia aliyokuwa akilipwa na anayotakiwa lipwa haikutathiminiwa kwa uchunguzi zaidi,tarehe 4/Desemba/2018 , Mahakama kuu ikatoa uwamuzi wake ,kwa kutupilia mbali ombi la Serikali kwa gharama (with costs),kwa sababu ya kuwa nje ya muda na sababu zingine.

Kwani ni siku 30 tuu ndio limit ya kuomba kukata rufaa iliku-review maamuzi ,ila tangu 2010 hadi 2018 siku 2,632 zilikuwa zimekatika,pia nyongeza ya muda ni siku 21 ,wakiongeza mara nyingine ni siku 42 ambazo wazi tulikuwa nje ya muda.

Kuanzia hapo baada ya ombi kutupiliwa mbali ,akina Prof.Kabudi kama waziri wa sheria na AG wakafikiri kufanya mabavu.

Tarehe,12/March /2019 .Bwana Steyn alituma email kwa Prof.Kabudi ikisema hivi sehemu ya ujumbe " I have been thrown out of the country ,and am unable to talk to any one in the government ,l have no option but to seek help outside Tanzania *This is something ,l never wanted*" alimwambia Prof. kabudi kuwa amezuiwa kuingia nchini ,hivyo hawezi kupata nafasi kuongea na kiongozi yeyote serikalini ,hana namna zaidi ya kutafuta haki yake nje ya Tanzania,ingawa ni kitendo ambacho hakupenda kutafutia haki nje ya Tanzania .

Akina prof.Kabudi wakampuuza , huku wakihubiri *Tanzania ni nchi huru*, *Vita ya kiuchumi* ,wanashindwa kujua kuwa mataifa yetu haya hayapo huru kwa namna anavyo hubiri kila siku.

Unapoingia mikataba na nchi zingine yaani (Multilateral na bilateral treaties) ,unapokubali kuwa mwanachama wa mahakama za usuluhishi kimataifa ,au sheria zingine za kimataifa, kama taifa huwezi kusema upo huru kuamua unavyotaka wewe .

Kuna sheria inaitwa *Unified enforcement of foreign Judgement act/law*  yaani sheria ambayo Mahakama ya nchi wanachama inaweza kuridhia kutekeleza hukumu au maamuzi ya mahakama ya nchi nyingine wanachama.SADC tunayo hiyo sheria inaitwa *Mutual reciprocal enforcement of judgements* .South Africa ni mwananchama wa SADC ,Steyn alivyosema anatafuta msaada nje,akina Kabudi walimpuuza.

Steyn akachukua Arbitral awards na hukumu alizoshinda huku Tanzania ,akazipeleka Mahakama ya Afrika kusini ambayo ni sehemu ya SADC .

 Maamuzi ya mahakama ya Afrika ya kusini yakatoka *NDEGE YETU KUKAMATWA* ,kosa ni la nani kama sio la Prof.Kabudi na AG ? ,hawakujua kama kuna hiyo sheria ya maamuzi ya mahakama ya ndani  kuwa executed , mahakama ya nje nchi wanachama?

kwanini walimzuia Steyn kuingia ndani ya nchi ? ,kama aliridhia kupunguza kutoka USD Mil 36 hadi USD Mil 30 ,je tulishindwa kuongea apunguze hiyo ,USD mil 9 ,iliyokuwa imebaki?

Sasa hilo deni USD Mil 9 ndio inafidia ndege yetu ya mabilioni? ,kwa maamuzi yao hayo yamesaidia Taifa au yame angamiza taifa ?,tuwe wakweli kwa maslahi ya taifa letu. 

Tuwe wakweli ,nchi yetu ndio ipo huru ila huwezi kusema tupo huru kwa wewe kufanya unachotaka ,bila kujua Tanzania tumeridhia mikataba mingi ya kimataifa inayolinda wawekezaji hawa,mfano.MIGA rules  (Multilateral investment Guarantee Agency),ICSID rules (International center for settlement of disputes),IFC rules (International finance corporation), UNCTTRAL(united nation Commission on international Trade laws),tuna bilateral treaties 26 .

Sheria hizi zinawalinda sana,na sisi tumeziridhia ,hivyo katika kupigania maslahi ya taifa letu kama viongozi ,lazima pia mkumbuke kuwa kuna hizi sheria ,tukifanya ubabe au tunavyotaka bila kufuata taratibu , wataendelea kufungua kesi nje kupitia sheria hizi ,kesi zitatolewa maamuzi nje , wataendelea  kusubiri ndege zetu huko huko kila kukicha ili kuzimamata.

Je,mtafuata ushauri wa Musiba tuvunje safari za huko ughaibuni ? ,ili ndege zetu zisikamatwe? ,basi hapo ndio mtapaswa kufungwa kabisa kwa uhujumu uchumi tena bila dhamana.

Katika hili Prof.Kabudi  na AG kwanini wasishtakiwi kwa kuhujumu taifa letu ?.

Abdul Nondo

abdulnondo10@gmail.com




No comments :

Post a Comment