Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, September 25, 2019

Dk. Shein atembelea kiwanda cha Kampuni ya Kimataifa ya Utafiti na Uchimbaji wa Mafuta!

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein ametembelea kiwanda cha Kampuni ya Kimataifa ya Utafiti na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia  ya Ras Al Khaimah “RAK GAS” iliyopo nje kidogo ya mji wa Ras Al Khaimah na kujionea shughuli za kiwanda hicho.

Katika kiwanda hicho ambacho kimekuwa kikifanya shughuli mbali mbali za kupokea gesi kutoka katika maeneo maalum ya uchimbaji, kuisambaza sambamba na kuihifadhi kwa lengo la kuweza kuitumia.

Akiwa na ujumbe wake, Dk. Shein alipata maelezo kutoka kwa viongozi wa Kampuni hiyo ya Kimataifa ya Utafiti na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia  ya Ras Al Khaimah “RAG GAS” akiwemo Meneja Mkuu Peter Deibel, Msaidizi Meneja Mwendeshaji  Jody Labbie na Mwangalizi Mkuu wa Uzalishaji Deepu Thomas ambaye alitoa ufafanuzi juu ya uzalishaji pamoja na usambazaji wa gesi asilia kiwandani hapo.
Rais Dk. Shein alieleza kuvutiwa na shughuli mbali mbali zinazofanywa na kiwanda hicho katika eneo hilo lililopo nje kidogo ya mji wa Ras Al Khaimah ambalo ni muhimu katika shughuli za gesi asilia ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Ras Al Khaimah.

Alipongeza hatua kubwa za maendeleo pamoja na mchango mkubwa wa mradi huo wa gesi kwa uchumi na maendeleo ya Ras Al Khaimah unatokana na mikakati madhubuti iliyowekwa katika kuhakikisha juhudi hizo zinachangia na kuendeleza soko la ajira, ukuaji wa uchumi na maendeleo ya viwanda katika nchi hiyo.

No comments :

Post a Comment