Nyakati zile enzi Ujerumani imegawanyika, kulikuwa na ukuta mkubwa wa Berlin unaozitenganisha Ujeremami Mashariki na Ujerumani Magharibi.
Siku moja baadhi ya watu wa Ujerumani Mashariki walijaza gari taka lenye kila aina ya uchafu na kuutupia upande wa pili wa ukuta.
Watu wa Ujerumani Magharibi wangeweza kuwarudishia kwa kutupa uchafu upande wa pili tena hata zaidi. Kilichowashangaza wengi ni kuwa badala ya kurejesha matakataka wao waliamua kutuma madikodiko kama vile mikate, maziwa, nyama za kopo na mazagazaga kibao kisha wakayaweka kwenye package safi na kuyaweka upande wa pili. Lakini juu ya mzigo waliouweka upande wa pili wakaandika bango kubwa linalosomeka:
"KILA MMOJA HUTOA ALICHONACHO"
Maneno haya sio tu yaliwaumiza waliotupa matakataka bali yaliwafanya wajione hawafai kwa kila kitu. Ilikuwa ni kisasi cha akili.
Jiulize, Je, wewe una nini ndani yako?
Upendo au Chuki?
Vurugu au Amani?
Uhai au Umauti?
Uwezo WA kujenga ama Kubomoa?
Je, Umejifunza nini? "KILA MMOJA HUTOA ALICHONACHO"
Fikiria, Jifunze....
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
No comments :
Post a Comment