Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, September 4, 2019

Mripuko waharibu majengo matatu na kujeruhi watu Antwerp Ubelgiji!

Watu chungunzima wamejeruhiwa na wengine wamenasa kwenye majengo kadhaa baada ya mripuko kuutikisa mji wa bandari wa Antwerp nchini Ubekgiji.

Taarifa hizo zimetolewa na polisi waliosema mripuko huo umeyaathiri majengo matatu katika wilaya ya Wilrijk eneo la kusini mwa katikati ya mji.

Kufikia sasa watu wawili wameokolewa kutoka kwenye kifusi kwa mujibu wa taarifa za zima moto zilizoandikwa kwenye ukurasa wa Twitta na kuongeza kwamba wanajitahidi kumuokoa mtu wa tatu.
Mbwa wa kunusa wanatumiwa kufuatilia watu waliotoweka katika mkasa huo.Hakuna taarifa za mara moja zilizotolewa na polisi kuhusu kilichosababisha mripuko huo uliotokea mchana,ingawa meya wa Antwerp Bart de Wever ameandika kupitia Twitta kwamba ni mripuko wa gesi.

No comments :

Post a Comment