Rais wa Iran Hassan Rouhani leo ameondowa uwezekano wa kufanya mazungumzo yoyote ya moja kwa moja na Marekani na kutishia kuchukua hatua zaidi ya kupunguza ushirikiano wa Iran katika makubaliano ya nyuklia katika kipindi cha siku kadhaa.
Rohani ameyazungumza hayo katika hotuba yake aliyoitowa mbele ya bunge na kusema kwamba mazungumzo ya aina yoyote na Marekani yatabidi kufanyika chini ya utaratibu wa kundi la nchi zenye nguvu zilizotia saini makubaliano ya kihistoria ya nyuklia na Iran mwaka 2015.
Rais huyo wa Jamhuri ya kiislamu ya Iran pia amebaini kwamba nchi yake iko tayari kupunguza ushirikiano katika makubaliano hayo ndani ya siku zijazo ikiwa mazungumzo na nchi za Umoja wa Ulaya hayatozaa matunda kufikia Alhamisi.
Iran na Marekani ziko katika mkwaruzano tangu mwezi Mei mwaka jana baada ya rais Donald Trump kuchukua hatua ya kivyake ya kujitenga na makubaliano na kuanza kuiwekea tena vikwazo vikali Iran.

No comments :
Post a Comment