Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 13, 2019

Umoja wa Mataifa wamkosoa Netanyahu!

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kwamba ahadi ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwamba atalinyakua kwa mabavu eneo la bonde la Jordan itasababisha ukiukaji mkubwa wa sheria ya kimataifa.

Tamko hilo kali la Umoja wa Mataifa la kumpinga Netanyahu limekuja kufuatia msururu wa kauli za kumkosoa waziri mkuu huyo kutokana na ahadi aliyoitowa ya kutaka kulinyakua kwa mabavu eneo hilo la ardhi ya Wapalestina ikiwa atachaguliwa tena wiki ijayo.
Katika taarifa msemaji wa Antonio Guterres, Stephane Dujarric pia ameeleza kwamba ahadi ya Netanyahu itakuwa ya uharibifu wa harakati za uwezekano wa amani na wapalestina.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa imesema baada ya Saudi Arabia,nchi yenye nguvu katika kanda hiyo na ambayo imekuwa na uhusiano wa karibu na Israel katika kipindi cha karibuni,kulaani hatua inayopangwa na Netanyahu.

Kadhalika wizara ya mambo ya nje ya Urusi imelaani hatua hiyo kabla ya mkutano baina ya Netanyahu na rais Vladmir Putin unaofanyika leo.

No comments :

Post a Comment