Waziri wa Habari na Mambo ya kale Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo amesema Serikali ya Zanzibar (SMZ) kwa kushirikiana na wadau wa utaliii wameandaa mafunzo maalumu ya uongozi kwa vijana wa wazawa ambayo yatawawezesha kushika nafasi za juu katika hoteli na kampuni za kitalii zilizopo Nchini.
Amesema mafunzo hayo yameandaliwa mara baada ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanibar (SMZ) kubaini kuwa katika Mahoteli makubwa na kampuni za Kitalii zilizopo Nchini nafasi za juu za uongozi zinashikwa na wageni.
Kauli hiyo ameitoa leo Septemba 25 katika Ufungaji wa mafunzo maalumu ya siku 3 kwa vijana 40 wazawa kutoka Kampuni na Taasisi mbali mbali zinazoshughulika na Utalii visiwani Zanzibar.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na wakufunzi kutoka nje ya Nchi kwa vijana ambao tayari wameshaajiriwa katika Hoteli na kampuni mbali mbali za kitalii zilizopo Nchini
Mahmoud Thabit Kombo alisema kumekuwepo na wimbi la wageni wengi kama vile wazungu na wahindi kushika nafasi za juu katika hoteli na kampuni za kitalii wakati nafasi hizo zinaweza kuongozwa na vijana wazawa.
“Ukweli kuwa hoteli nyingi Zanzibar zile nafasi ya juu zinaongozwa na wageni licha ya kuwa nafasi hizo hizo zinaweza kuongozwa na vijana wetu wazawa” Alisema Waziri kombo.
Alisema kwa kuliona hilo Serikali imeamua sasa kuwanoa vijana hao wazawa ambao wanauwezo ili kushika nafasi hizo ili nao kunufaika na utalii uliopo nchini kwao.
“Wageni hushika nafasi za juu na kulipwa fedha nyingi sana wakati nafasi kama hizo kuna wanzanzibar na watanzania wanaweza kuziongoza fedha zikabaki nchini navijana wetu wkanufaika” alisema Waziri.
Katika maelezo yake alisema kuwa Serikali itaendelea kupanga mipango mbali mbali kwa lengo la kukua utalii na kuwainua vijana kiuchumi kupitia Sekta ya utalii.
Waziri alieleza kuwa katika juhudi za kukuza utalii wa Zanzibar na kuwainua vijana serikali imeleta watalaamu kuja kufanya utafiti wapi Zanzibar inakosea na wazawa washike nafasi za juu katika kampuni za kitalii.
“Tayari utafiti umefanywa umegundua mambo mengi moja vijana wetu wanapo kuwa vyuoni wasoma kwa lengo kufaulu mitihani tu, ukiwaweka katika mazinira ya kazi hawawezi kukifanyia kazi kile walichokisoma” alieleza Waziri.
Aidha alieleza kuwa mbali nahilo utafiti huo umebaini kuwa vijana wengi hawana ujasiri wa kujiamini pndi wwanapofanyiwa usaili wa kazi.

No comments :
Post a Comment